img

Waandamanaji Thailand wamtaka Waziri Mkuu aondoke

November 27, 2020

 

Maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya Thailand wametoa wito wa kumalizika kwa mapinduzi katika nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia siku ya Ijumaa wakati miezi kadhaa ya maandamano ya mitaani ikizusha tetesi za kutokea mapinduzi mengine ya kijeshi. 

Waandamanaji wanamtaka kujiuzulu Waziri Mkuu Prayuth Chan-ocha, jenerali wa zamani wa kijeshi aliyekamata madaraka katika mapinduzi ya mwisho mwaka wa 2014, lakini wanasema hawataki nafasi yake ichukuliwe na jenerali mwingine. 

Waandaaji wameyaita maandamano ya leo “Mazoezi ya Kupinga Mapinduzi”. Mapinduzi yaliyoongozwa na Prayuth yalikuwa ya 13 ya kijeshi nchini humo tangu kumalizika kwa utawala wa mamlaka ya Kifalme mwaka wa 1982.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *