img

Uchaguzi wa Marekani 2020: Trump aonyesha ishara za kuwa tayari kuondoka Ikulu

November 27, 2020

Dakika 5 zilizopita

Trump akiingia ndani ya ndege ya Airforce one
Maelezo ya picha,

Trump akiingia ndani ya ndege ya Airforce one

Rais Donald Trump wa Marekani amesema ataondoka Ikulu ikiwa Joe Biden atathibitishwa rasmi kuwa rais anayefuata wa Marekani kwa kura za wajumbe.

Raia amekataa kukubali alishindwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 3 na kuwaambia wanahabari Alhamisi itakuwa vigumu kwake kukiri kushindwa.

Pia kwa mara nyingine tena amedai uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura. Bwana Biden anaongoza kura za wajumbe kwa kupata 306 huku Trump akiwa na kura 232.

Kura alizopata Bwana Biden zikiwa zimepita 270 idadi inayohitajika kwa mgombea kuwa rais wa Marekani.

Bwana Biden pia anaongoza kwa wingi wa kura kwa zaidi ya milioni 6.

Wawakilishi wa kura za wajumbe watakutana mwezi ujao kuidhinisha rasmi kura zilizopigwa huku Joe Biden wa chama cha Democratic akisubiri kuapishwa kuwa rais Januari 20.

Rais na wafuasi wake wamewasilisha kesi kadhaa wakipinga uchaguzi lakini nyingi zimetupiliwa mbali.

Mapema wiki hii, Bwana Trump hatimaye alikubali kuruhusu kuanza kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa rais mteule Joe Biden baada ya wiki kadhaa za sintofahamu.

Uamuzi huo unamaanisha Bwana Biden anaweza kupata taarifa za usalama wa nchi na kuwasiliana na maafisa wa juu serikalini pamoja na kuweza kutumia mamilioni ya madola wakati anajitayarisha kuchukua rasmi madaraka Januari 20.

Trump alisema nini?

Alipoulizwa Alhamisi ikiwa atakubali kuondoka Ikulu ya Marekani kama alishindwa katika kura za wajumbe, alisema: “Bila shaka nitaondoka, nitaondoka na munajua hivyo.”

Hata hivyo, aliendelea kusema kuwa “ikiwa watamchagua [Joe Biden], wamefanya makosa”, na kuonesha kana kwamba huenda asikukubali matokeo.

“Itakuwa jambo gumu sana kukubali kushindwa kwasababu tunajua kulikuwa na wizi mkubwa wa kura,” amesema, madai ambayo amekuwa akiyataja kila wakati bila kutoa ushahidi.

Aidha, hakusema ikiwa atahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Biden.

Mchakato wa kawaida wa kukabidhi madaraka kutoka kwa rais mmoja hadi mwingine na kuthibitisha kuwa ameshindwa ni jambo ambalo rais Trump amekuwa akipinga.

Chini ya mfumo wa kura za wajumbe nchini Marekani, wapiga kura sio wanaomchagua rais moja kwa moja. Badala yake, kuna maafisa 538 wanaopiga kura ambao wamegawanywa katika majimbo mbalimbali Marekani kulingana na idadi ya watu katika jimbo husika.

Joe Biden

Bwana Biden tayari ametangaza maafisa wake wa ngazi ya juu baada ya yeye kuchukua madaraka rasmi kutoka kwa Donald Trump Januari, na amesema ushirikiano wa kukabidhi madaraka kutoka Ikulu umekuwa wa kweli.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *