img

Polisi wasimamishwa kazi Ufaransa kwa kumpiga mtu mweusi

November 27, 2020

Dakika 5 zilizopita

French music producer, identified only as Michel, talking to the media outside the IGPN (France's National Police General Inspectorate)

Tukio hilo lililofanyika siku ya Jumamosi na kuitibua malalamiko mapya kuhusu mienendo ya vikosi vya usalama.

Polisi walituhumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuvunja kambi ya muda ya wahamiaji mjini Paris.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo serikali inajaribu kutekeleza sheria kupiga marufuku matangazo yanayoonesha nyuso za maofisa wa polisi.

Wakosoaji wa sheria hiyo wanasema kwamba bila ya kuwa na picha kama hizo, visa kama vile vilivyotokea wiki zilizopita visngejulikana.

Mamlaka nchini Ufaransa zimewasimamisha kazi maofisa watatu wa polisi baada ya kuonekana katika kanda ya video wakimpiga mtayarishaji wa muziki mweusi mjini Paris.

Siku ya Alhamisi, mchezaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, ambaye ni mweusi, aliungana na wachezaji wenzake wa taifa na wanaridha kulaani kisa cha hivi punde.

“Video hii inashangaza sana, ghasia kama hizi hazitakubalika. Tunakataa ubaguzi wa rangi,”aliandika katika mtandao wake wa Twitter na akaweka picha iliyo na uso uliojaa damu ya mtayarishaji muziki huyo aliyejeruhiwa, ambaye jina lake lilitajwa kama Michel tu.

Video za camera za siri ilichapishwa siku ya Alhamisi katika mtandao wa habari wa Loopsider.

Inawaonesha maofisa watatu wa polisi wakimpiga mateke na ngumi mtu huyo baada ya kuingia studio.

Loopsider alisema awali alisimamishwa kwa kutovalia barakoa.

White spacer

Michel alisema kuwa alishambuliwa kwa kutumia maneno ya kibaguzi wakati wa kichapo hicho kilichodumu dakika tano.

Alizuiliwa na kushtakiwa kwa kuzua ghasia na kukataa kukamatwa, lakini waendesha mashtaka walitupilia mbali mashtaka hayo na badala yake kuanzisha uchunguzi dhidi ya maofisa hao.

Alipofika kituo cha polisi siku ya Alhamisi akiwa na wakili wake kuandikisha malalamishi, Michel aliwaambia wanahabari: “Watu ambao walitakiwa kunilinda walinishambulia. Sikufanya lolote kushtahili kutendewa hivyo. Kile ninachotaka ni maofisa hao watatu kuchukuliwa hatua kisheria .”

Meya wa Paris Anne Hidalgo amesema “ameshtushwa sana na kitendo hicho”.

Waziri wa wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin ameambia kituo cha televisheni cha Ufaransa kwamba atashinikiza maofisa hao ‘ kufutwa kazi, akisema kitendo chao “kimeharibia sifa ya idara ya polisi ya nchini”.

Mapema wiki hii Bwana Darmanin aliamuru polisi kutoa ripoti kamili baada ya kubolewa kwa lazima kwa makazi ya muda ya wahamiaji katika mji mkuu, baada ya makabiliano kuzuka kati ya wahamiaji na wanaharakati

Aliandika katika Twitter yake akisema baadhi ya picha kutoka eneo la tulip ni za “kushangaza”.

Huku hayo yakijiri, serikali ya Ufaransa inaendelea na mbele na mswada tata wa usalama, ambao wapinzani wanasema huenda ukahujumu uweze wa vyombo vya habari kuchunguza mienendo ya polisi.

Kifungu cha 24 cha mswada huo kinaharamisha kuwekwa mtandaoni kwa picha ya polisi au askari, hatua ambayo inaonekana kuwalenga wao binafsi.

Serikali inasema kuwa mswada huo mpya haukiuki haki ya vyombo vya habari na raia wa kawaida kuripoti dhuluma za polisi.

Lakini licha ya ukosoaji huo serikali imefanyia marekebisho mswada huo, na kufafanua kuwa kifungu cha A 24 “kitalenga tu uchapishaji wa picha ambao unaonesha wazi lengo lake ni kumdhuru afisa wa polisi kimwili au uadilifu wa kisaikolojia “.

Watu watakaopatikana na na makosa huenda wakafungwa jela mwaka mmoja au kutozwa faini ya hadi €45,000 (£40,000).

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *