img

Mzozo wa Tigray Ethiopia: Waziri Mkuu Abiy Ahmed ni nani?

November 27, 2020

Dakika 5 zilizopita

Abiy Ahmed

“Kwa mtazamo wangu, Siamini Ethiopia inahitaji vita. Sitaki kujumuishwa miongoni mwa watu wanaopendelea suluhisho la kijeshi.

Kile ninachotaka kutuma Tigray sio risasi, afadhali nitume barakoa [ambayo inaweza kutumiwa kujikinga dhidi ya] virusi vya corona”.

Hiyo ilikuwa kauli ya Waziri Mkuu Abiy mwezi Septemba wakati jimbo la Tigray linaloongozwa na TPLF iliamua kufanya uchaguzi kupinga amri iliyotolewa na serikali kuu.

Uchaguzi ulikuwa umeahirishwa kutokana na janga la corona.

Wakati huo alisema serikali haitakabiliana kijeshi na jimbo hilo la kaskazini.

Leo Waziri Mkuu anaongoza oparesheni dhidi ya uongozi wa TPLF.

Mzozo huo ambao umeingia wiki ya tatu umeripotiwa kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Mashirika ya kutoa misaada ya binadamu yanasema maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko zaidi ya watu elfu arobaini wakitorokea nchi jirani ya Sudan.

Umoja wa Mataifa umeonya kutokea kwa mzozo wa kibinadamu.

Abiy Ahmed aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia mwezi Aprili mwaka 2018, kufuatia wimbi la maandamano kutoka jamii ya Oromo.

Nchi ilisemekana kuwa katika hatari ya kukabiliwa na mapigano ya wenyewe kwanza wenyewe.

Cheering supporters of PM Abiy

Aliamua kuleta mageuzi makubwa, baadhi ya mageuzi hayo hayakutarajiwa miaka michache iliyopita.

Kwa miaka mingi, serikali ya Ethiopia imekuwa ikikosolewa na makundi ya kutetea haki kwa ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, kuwatenga na kuwafunga viongozi wa upinzani na kutumia nguvu kuvunja maandamano.

Pia ilionekana kupinga uamuzi wa tume ya mipaka ambao ulitarajiwa kukomesha mzozo wa miongo miwili kati yake na nchi jirani ya Eritrea.

Lakini hayo yote yalibadilika Abiy alipoingia madarakani. Alikubaliana na uamuzi huo na kufikia mkataba wa amani na Eritrea.

Uamuzi huo wa kihistoria ulimwezesha kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2019.

Alionekana kujitolea kikamilifu kufikia amani na ‘maadui’ wa watangulizi wake.

Baba yake Ahmed Ali ambaye alifariki dunia mwaka mmoja baada ya yeye kuwa waziri mkuu alimuelezea kama ”mtoto ambaye alikuwa rafiki wa kila mtu ,” katika mahojiano na BBC mwezi Julai mwaka 2018.

Abiy Ahmed ni nani?

Abiy Ahmed at a rally

Historia ya Bwana Abiy ni muhimu katika kutathmini jinsi watu wanavyomchukulia.

Ni kiongozi wa kwanza kutoka jamii ya Oromo nchini humo – Kabila ambalo liliongoza maandamano ya kupinga serikali kwa karibu miaka mitatu, na kusababisha vifo vya watu kadhaa na maelfu ya wengine kukamatwa kufuatia makabiliano na vikosi vya usalama.

Moja ya malalamiko makuu ya waandamanaji ni kwamba wametengwa kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa miaka mingi- licha ya kuwa jamii iliyo na watu wengi zaidi nchini humo.

Bwana Abiy alipoingia madarakani, hayo yote yalainza kubadilika.

Aliwahi kuwa kuwa kiongozi wa Oromo People’s Democratic Organisation (OPDO), moja wapo wa vyama vinne vikuu vya kijamii ambavyo viliungana kubuni muungano wa chama tawala cha Ethiopian People’s Revolutionary Democratic Front (EPRDF) .

Mwezi Desemba mwaka jana, Bwana Abiy alivunjilia mbali EPRDF ambayo imeongoza siasa za Ethiopia kwa karibu miongo mitatu, na kubuni chama kimoja cha kitaifa, Prosperity Party, chama ambacho TPLF ilikataa kujiunga.

he leader of the "Oromo Peoples Democratic Organization" (OPDO) Abiy Ahmed looks on during a news conference in Aba Geda, Ethiopia, 02 November 2017

Waziri Mkuu huyo aliye na umri wa miaka 44 – alizaliwa katika mji wa Agaro ulioko jimbo la Oromia anatoka katika familia mchanganyiko wa Wakristo Waislamu, alijiunga OPDO mwishoni mwa miaka ya 1980.

Katika jeshi alipanda madaraka na kufikia cheo cha luteni kanali, kabla ya kuwa mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika la mawasiliano na usalama, mtandao ambao jukumu lake lilikuwa kutoa huduma ya usalama wa kimtandao katika nchi ambayo serikali inadhibiti vikali intaneti.

Baada ya hapo alikuwa waziri wa sayansi na teknolojia.

Ameahidi kuweka mabadiliko katika mawasiliano ya simu, ambayo ambayo kwa sasa inaendeshwa na serikali.

Celebrations as border is reopened

Presentational grey line

Maelezo muhimu: Abiy Ahmed

Abiy Ahmed

Alizaliwa mjini Agaro kusini mwa Ethiopia mnamo Ahosti 15, mwaka 1976 katakana na baba Muoromo Muislamu na mama Mkristo kutoka jamii ya Amharic.

Mwaka 1990 akiwa kijana barobaro, alijiunga na harakati za kijeshi dhidi ya utawala wa kimila wa Derg.

Ana shahada ya uzamifu ya masala ya Amani na usalama kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa na shahada ya uzamili ya katika masala ya uongozi kutoka chuo kikuu cha Greenwich, London.

Anazungumza lugha ya Kioromoo, Amharic ,Tigrinya, na Kiingereza.

1995: Alihudumu kama Melinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda

2007: Alibuni shirika la Ethiopia la mawasiliano na usalama wa mtandaoni (INSA) na kuhudumu kama mwanachama wa bodi ya Ethio Telecom, Ethiopian TV

2010: Aliingia katika siasa kama mwanachama wa kawaida wa OPDO kabla ya kujiunga na makakati juu ya chama hicho mwaka 2015

2016: Alihudumu kwa muda mfupi kama waziri wa sayansi na teknolojia.

2018: Alikuwa Waziri Mkuu

2019: Aliunganisha muungano wa chama tawala EPRDF, ikuwa chama kimoja – cha Prosperity Party.

2019: Alishinda Tuzo ya Amani ya NobeL.

2020: Alitangaza opqaresheni ya kijeshi dhidi ya TPLF

line

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *