img

Mwanadiplomasia wa Iran kushtakiwa Ubelgiji kuhusu jaribio la bomu

November 27, 2020

Mjumbe wa kidiplomasia wa Iran anafikishwa mahakamani leo nchini Ubelgiji akituhumiwa kwa kupanga shambulizi la bomu katika mkutano wa upinzani nje ya mji mkuu wa Ufaransa, Paris, katika kesi ambayo imezusha mivutano na Iran. 

Assadollah Assadi, ambaye wakati mmoja alihudumu mjini Vienna, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela kama atapatikana na hatia. 

Mnamo Juni 2018, maafisa wa Ubelgiji walizuia kile walisema ni jaribio la kuingiza mabomu nchini Ufaransa kwa njia ya magendo ili kuushambulia mkutano wa mojawapo ya mavuguvugu ya wapinzani wa Iran wanoishi uhamishoni. 

Kesi dhidi ya Assadi, inakuja siku moja baada ya kufanywa mpango wa kubadilishana wafungwa, ambapo Wairan watatu waliofungwa jela kuhusiana na njama ya shambulizi la bomu nchini Thailand mwaka wa 2012 waliachiwa, kwa kubadilishana na mhadhiri wa Kiaustralia mwenye asili ya Uingereza aliyefungwa jela na Iran kwa madai ya upelelezi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *