img

Msemaji wa serikali ya Iraq ajiuzulu

November 27, 2020

Msemaji wa Serikali ya Iraq Ahmed Molla Talal, ametangaza kujiondoa kwenye wadhifa wake wa kikazi.

Talal alitoa maelezo na kuarifu,

“Kazi yangu ilikuwa nyeti inayohitaji uangalifu sana. Nafasi hii ya kazi nilikabidhiwa na kiongozi wa kitaifa na mwenye roho safi na nia njema  (Waziri Mkuu Mustafa al-Kazimi).”

Talal aliongezea kusema kuwa ataendelea kuitumikia nchi katika maeneo mengine na nyanja tofauti.

Kulingana na taarifa za vyanzo vya serikali, Ahmed Molla Talal anatarajiwa kuteuliwa kama balozi wa moja ya nchi za Ghuba katika siku zijazo.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *