img

Meli kubwa ya mizigo yatia nanga bandari ya Tanga

November 27, 2020

Meli kubwa ya Mizigo iliyobeba tani 55,000 za klinka kutoka nchini Dubai, imetia nanga katika bandari ya Tanga baada ya kukamilika kwa uongezwaji wa kina katika awamu ya kwanza ikiwa ni jitihada za Serikali ya awamu ya tano za kuboresha bandari hiyo iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 256 kwaajili ya Maboresho hayo.

Bandari ya Tanga ni bandari ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na bandari ya Dar es salaam. Miongoni mwa viongozi walioshuhudia meli hiyo ikitia nanga ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu ambae anawasisitiza wananchi kuchangamkia fursa za ajira zitakazojitokeza.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *