img

Mbunge Sanga kutimiza ndoto za vijana Makete, Aahidi kusomesha 10 kila mwaka VETA

November 27, 2020

Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga ameahidi kuwasomesha vijana 10 kila mwaka katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA kilichopo Makete.

Akizungumza katika mahafali ya Chuo hicho leo, Sanga amesema ataanza kuwalipia ada vijana 10 wanaotoka kwenye kata mbalimbali za Makete ambao watakua ni wale wenye uhitaji na wanaotoka kwenye mazingira magumu ya kiuchumi.

” Mimi kama Mbunge nitaanza kuwalipia ada vijana 10 tutaandaa utaratibu mzuri wa kuwapata lengo ni kuhakikisha tunakua na Vijana wengi wenye ujuzi na fani mbalimbali ambao hata wakisaidiwa mikopo wana uwezo wa kujiajiri lakini pia kupitia mafunzo watakayopata hapa yatawawezesha kupata ajira sehemu mbalimbali.

Inasikitisha kuona kati ya wanafunzi 64 wanaohitimu leo wanafunzi wanaotokea hapa Makete hawafiki 10 zaidi ya 50 wanatoka nje hii maana yake tunashindwa kutumia fursa, niwaombe sana ndugu zangu tuitumie fursa ya kupata Chuo hiki ili vijana wetu wafaidikie nayo,” Amesema Sanga.

Sanga ameipongeza serikali kwa kujenga Chuo hiko kikubwa na cha kisasa mkoani Njombe ambacho kina mazingira mazuri na vifaa vya kisasa huku akiahidi kuwa balozi mzuri wa kukitangaza.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *