img

Kenya yapunguza idadi ya wageni wanaohudhuria harusi kutokana na corona

November 27, 2020

dadi ya wageni watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi nchini Kenya imepunguzwa hadi kufikia watu 50 pekee kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Baraza linalojumuisha dini mbali mbali nchini humo limesema kuwa chakula kinachotolewa katika harusi kitakuwa kikitilewa kwa wazazi na ndugu wa damu wa maharusi pekee.

Mwezi Agosti Rais Uhuru Kenyatta aliongeza idadi ya wageni wanaoweza kuhudhuria harusihadi watu 100 alipolegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Katika masharti mapya yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii, chakula kimepigwa marufuku katika mazishi na idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi imepunguzwa hadi watu 100 pekee.

Muda wa mazishi pia umerekebishwa kwa kupunguzwa hadi saa moja pekee.

Huduma za kanisa pia hazitatolewa kwa zaidi ya dakika 90.

Wiki iliyopita mwenyekiti wa baraza la dini mbali mbali nchini Kenya, Anthony Muheria, alitibiwa virusi vya corona katika hospitali moja mjini Nairobi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *