img

Halmashauri kununua gari ya mkurugenzi ya milioni 400, mbunge Msukuma ataka ichunguze

November 27, 2020

Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Kasheku maarufu Musukuma amemtumia salamu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kufuatia halmashauri hiyo kufanya manunuzi ya magari likiwemo Gari la Mkurugenzi Toyota V8 lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 400 ambapo amedai manunuzi hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

Musukuma ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Waadishi wa habari Mkoani Geita ambapo amedai mchakato wa manunuzi haujapewa baraka na vikao vya Baraza la madiwani katika Halmashauri hiyo na ni kwenda kinyume na matumizi ya fedha za SCR zinazotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGML.

Na ameenda mbali zaidi na kuiomba Serikali kutuma tume ya Uchunguzi kwenye halmashauri hiyo ili kubaini kama mchakato huo ulifuata hatua za kisheria.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *