img

Diego Maradona: Mchejzaji nyota wa Argentina azikwa huku Argentina ikiomboleza

November 27, 2020

Dakika 7 zilizopita

Umati mkubwa wa watu wakihudhuria mazishi ya Maradona
Maelezo ya picha,

Umati mkubwa wa watu wakihudhuria mazishi ya Maradona

Mwanasoka Diego Maradona amefanyiwa mazishi katika sherehe ya kibinafsi katika mji wa Buenos Aires nchini Argentina siku moja baada ya kufariki dunia.

Jamaa na marafiki wa karibu tu ndio waliohudhuria mazishi yake.

Lakini awali, kundi kubwa la watu lilijitokeza kutoa heshima zao za mwisho wengi wakiwa wanabubujikwa na machozi na kuonesha upendo

Maradona alifariki dunia kwasababu ya mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 60.

Kifo chake kimesababisha watu kumuombeleza kote duniani lakini hakuna walioomboleza kama raia wa nchi yake waliomchukulia kama shujaa wa taifa.

Jeneza la Maradona lilifunikwa bendera ya taifa na fulana ya mpira nambari 10 nafasi aliyocheza uwanjani – pia fulana hiyo ilikuwa inaoneshwa kwa umma katika makao ya rais.

Kufikia mchana, foleni ya waliokuwa wamekuja kutoa heshima zao za mwisho ilifika umbali wa zaidi ya kilomita moja na polisi ikakabiliana na waombolezaji walipokuwa wanajaribu kufunga kwasababu ya muda.

Wengi waliomboleza kifo cha Maradona kwa njia tofauti

Maelezo ya picha,

Wengi waliomboleza kifo cha Maradona kwa njia tofauti

Aidha, kulikuwa na taarifa za waombolezaji kurushiwa mabomu ya kutoa machozi na risasi za mpira.

Mmoja wa waombolezaji aliona ni kana kwamba polisi wametumia nguvu kupitia kiasi.

“Tumepanga foleni bila fujo yoyote na ghafla polisi wakaanza kurusha risasi za mpira,” anasema, akinukuliwa na shirika la habari la Reuters. “Haifai, Mimi nataka tu umuaga Diego kwa mara ya meishi.”

Mashabiki wakipita kandokando ya jeneza la Maradona lililofunikwa bendera ya Argentina

Maelezo ya picha,

Baadhi ya mashabiki walipiga makofi wengine wakilia walipokuwa wakipita karibu na jeneza la Maradona

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *