img

COREFA yawaomba wadau kuzishangilia timu zao

November 27, 2020

 

Na Omary Mngindo, Bagamoyo.

CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA), kimewaomba wana-Pwani kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Kiembeni Fc Na Nyika Fc, zitazowakilisha mkoa kwenye michuano ya Azam Federation Cup (AFC).

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Simon Mbelwa, akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa ambapo amesema Jumamosi ya Nov 28 Kiembeni itacheza na Magereza ya Dar es Salaam katika uwanja wa Mwanakalenge.

Mbelwa alisema kwamba Disemba 3 Nyika Fc itaikaribisha Tandahimba Fc kutoka mkoani Lindi, katika uwanja wa JKT Ruvu (Mabatinil) Mlandizi ikiwa ni mwendelezo wa michuano hiyo ambapo Pwani inawakilishwa na vilabu hivyo viwili.

“Kiembeni ndio mabingwa wa wilaya ya Bagamoyo, ambapo katika mchezo wa awali iliifunga Msata United kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Mwanakalenge,” alisema Mbelwa.

Aliongeza kuwa Nyika ambao ndio mabingwa wa Mkoa wa Peani wao watashuka katika uwanja wa JKT Ruvu Mabatini ikiikaribisha Tandahimba, ambapo alisema hiyo ni fursa ya kipekee ya kuzishuhudia na kuziunga mkono timu hizo.

“Niwaombe wana-Pwani katika maeneo ya jirani na viwanja vitavyotumika kwa ajili ya michezo hiyo, kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu zetu ili ziweze kufanya vizuri kwenye kinyang’anyiro hicho kitakachompata mwakilishi wa nchi kwenye michuamo ya kimataifa,” alisema Mbelwa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mailimoja Kibaha mkoani Pwani Ramadan Lutambi alisema kuwa furda hiyo ni adimu na adhimu hivyo ni vyema kwa wana-Pwani wakazisapoti timu hizo ili ziwe wawakilishi kwenye michuano hiyo.

“Nina imani kubwa na timu zetu zinazoshiriki michuano hiyo hatua za awali zinaweza kufanya vizuti, kikubwa sisi wana-Pwani tuwe kitu kimoja katika kuzisapoti kwa kufika viwanjani, kwa waliombali waziombee hata dua,” alimalizia Lutambi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *