img

Barnier aelekea London kwa mazungumzo ya Brexit

November 27, 2020

 

Mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo ya Brexit Michel Barnier anaelekea London leo kufanya mazungumzo ya ana kwa ana ya kibiashara na mwenzake wa Uingereza David Frost, katika kile alichokieleza kuwa ni nafasi ya mwisho ya kupatikana muafaka. 

Barnier amesema kama Uingereza haitabadili msimamo wake, itakuwa vigumu sana kufikia makubaliano. Uingereza inaondoka katika eneo la biashara na forodha la Ulaya katika wiki tano zijazo, lakini mazungumzo yanayohusu makubaliano ya ziada bado yamekwama kuhusiana na haki za uvuvi na sheria za biashara ya haki. 

Uingereza imekuwa ikikataa kusaini mpango wa Umoja wa Ulaya wa mazingira sawa ya ushindani ya baada ya Brexit, kwa kuwepo na adhabu ya kibiashara kama kila upande utakiuka viwango vilivyokubaliwa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *