img

Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kupinga vitendo vinavyosababisha matendo ya ukatili wa kijinsia

November 26, 2020

Na Faruku Ngonyani , Mtwara

Kuelekea siku 16 za kupinga  matendo ya ukatili wa kijinsia  Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kuchukua hatua juu ya matendo hayo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Baltzari Komba Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Faidika Wote Pomoja (FAWOPA) shirika ambalo mara kadhaa limekuwa likishughuliki matendo hayo ya ukatali wa kijinsi Mkoani Mtwara.

Komba amesema kuwa kwa Mkoani Mtwara matendo yaliyokithili kwenye ukatili wa  kijinsi ni pamoja na ukatili kiuchumi ,ukatali wa kisaikolojia pamoja  na ukatili wa kimwili.

Aidha kuelekea siku 16 za kupinga matendo ya  ukatili wa kijinsi Mkoani Mtwara Shirika hilo la Fawopa limepanga kutoa elimu kwa jamii ili waweze kufahamu namna ya kukabiliana na matendo hayo ya ukatili wa kijinsia.

Lakini pia Komba ametoa wito kwa wananchi kuacha kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia haswa kwa upande wa wanawake na watoto.

“kuna ukatili wa kisaikolojia na imezoeleka katika jamii yetu kuwachukulia wananwake kama viumbe wa mapambo na wakati mwingine tumeona kwa baadhi ya wanaume wakiwasfia wanawake kwa kuwapigapiga kwenye maungo yao ,lakini pia kwa kumwangalia mwanamke na kumkonyeza ,haya pia ni matendo ya unyanysaji kwa wanawake”.

Ikumbukwe maadhimisho ya siku ya kupinga matendo ya ukatili wa kijinsi yataadhimishwa tarehe 10 Disemba 2020 kote nchini Tanzania

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *