img

Uingereza: Makubaliano ya biashara baada ya Brexit huenda kufikiwa

November 26, 2020

 

Waziri wa Fedha wa Uingereza, Rishi Sunak amesema nchi hiyo na Umoja wa Ulaya inaweza kufikia makubaliano ya biashara baada ya Brexit, japo nchi hiyo haitotia saini makubaliano kwa gharama yoyote ile.

Sunak ameliambia shirika la habari la Uingereza la Sky kuwa nia njema za pande zote itasaidia kufikia makubaliano hayo.Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen amesena leo kuwa umoja huo uko tayari kwa uwezekano wa Uingereza kuondoka katika umoja huo bila ya makubaliano mapya ya biashara.

Zikiwa zimebakia wiki tano pekee kwa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, pande zote zinajaribu kufikia makubaliano ya biashara ambayo yataepusha mgogoro zaidi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *