img

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 26.11.2020: Eriksen, Giroud, Szoboszlai, Alli, Winks, Musa

November 26, 2020

Dakika 6 zilizopita

Christian Eriksen

Arsenal wamepatiwa fursa ya kumsaini kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen katika makubaliano ya bei ya chini miezi 10 baada ya raia huyo wa Denmark , 28, kuondoka Tottenham. (ESPN)

Inter Milan itajaribu kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud , 34 kutoka Chelsea mwezi Januari. (Calciomercato – in Italian)

Arsenal inafikiria kumsaini kiungo wa kati wa Hungery Dominik Szoboszlai kutoka klabu ya Red Bull Salzburg na kumuuza kwa mkopo kwa klabu hiyo ya Austria kwa lengo la kuipiku RB Leipzig ya Ujerumani kutomsajili kiungo huyo.. (Football Insider)

Dominik Szoboszlai

Everton inawachunguza wachezaji watatu wa Tottenham kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari – kipa Paulo Gazzaniga, 28, Kiungo wa kati Delle Ali na Harry Winks wote wakiwa na umri wa miaka 24. (Football Insider)

Beki wa Ufaransa William Saliba, 19, yuko tayari kuwacha mshahara wa £90,000 kwa wiki ili kupata uhamisho wa mkopo kutoka Arsenal mwezi Januari. (Mirror)

Kiungo wa kati wa West Ham United na England Declan Rice, 21, anasema kwamba ni muhimu kushinda mataji licha ya uvumi kuhusu ombi la kutaka kumsajili kutoka Chelsea mwezi Januari.. (Metro)

Declan Rice

Mchezaji wa zamani wa England Jack Wilshere, 28, anasema kwamba itakuwa ndoto yake kujiunga na Arsenal baada ya kuachiliwa na Arsenal baada ya kuondoka West Ham. (Sun)

Sheffield Wednesday inajiandaa kumnunua aliyekuwa mchezaji wa Leicester City na Nigeria Ahmed Musa, huku mchezaji huyo wa Nigeria akiwa mchezaji huru baada ya kuachiliwa na klabu ya Al Nassr. (Football Insider)

Hatua ya klabu ya Real Madrid kumlenga Eduardo Camavinga imezua vita miongoni mwa mawakala huku mchezaji huyo wa Rennes na Ufaransa , 18 akivunja uhusiano na wakala wake. (AS – in Spanish)

Wakala maarufu Mino Raiola anasema kwamba wachezaji 300 huenda wakajiunga na Zlatan Ibrahimovic na Gareth Bale na kushtaki kampuni ya michezo ya EA Sports’ kwa kutumia watu kama wao katika michezo yao ya kanda za (Telegraph – subscription only)

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *