img

Mzozo wa Ethiopia: Waziri mkuu aamuru mashambulio dhidi ya mji wa Mekele

November 26, 2020

Dakika 6 zilizopita

ethiopia

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema ameanzisha “awamu ya mwisho” ya operesheni ya kijeshi katika jimbo la Tigray kwanza kushambulia mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.

Amesema wanajeshi watajaribu wasiwajeruhi raia na wito kwa watu katika mji huo kusalia majumbani mwao.

Hatua hilo inajiri baada ya muda wa mwisho uliyotolewa kwa wapiganaji wa Tigray kujisalimisha kumalizika siku ya Jumatano.

Chama cha TPLF, ambacho kinadhibiti mji wa Mekelle, kimeapa kuendelea na mapigano.

Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na maelfu ya wengine kutoroka makwao huku vikosi vya muungano vya Ethiopia vikiteka miji kadhaa ya Tigray kutoka kwa wapiganaji wa TPLF.

Hata hivyo ni vigumu kupata maelezo kuhusu mapigano hayo kwasababu mawasiliano ya simu na huduma za intaneti katika jimbo la Tigray yamekatizwa .

tygray

Mzozo huu unahusu nini?

Mwaka jana Bw Abiy alivunja muungano tawala , unaojumuisha vyama vilivyoundwa kwa misingi ya kikabila , na kuviunganisha katika chama kimoja, national party, the Prosperity Party, ambacho TPLF walikataa kujiunga.

Utawala wa Tigray unayaona mageuzi ya Bw Abiy kama jaribio la kujenga mfumo serikali moja na kuharibu mfumo uliopo sasa wa shirikisho.

Pia hukasirishwa na kile inachokiita urafiki wa waziri mkuu na rais wa Eritrea Isaias Afwerki “usiokuwa na kanuni “

Bw Abiy alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019 kwa juhudi zake za kuleta amani kwa kumaliza mzozo wa muda mrefu wa nchi yake na Eritrea.

ethiopia

Kwa upande wake, Waziri Mkuu anaamini kuwa maafisa wa TPLF wanahujumu mamlaka yake.

Bw Abiy alimuru mashambulio ya kijeshi dhidi ya TPLF baada ya kusema kuwa wapiganaji wake walikuwa wamevuka “mstari wa mwisho mwekundu”.

Aliwashutumu kwa kushambulia kambi ya kijeshi ya vikosi vya shirikisho tarehe 4 Novemba. TPLF walikanusha kuishambulia kambi ya majeshi.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *