img

Mahmoud Thabit kombo akabidhi ofisi

November 26, 2020

WAZIRI wa utalii na mambo ya kale Zanzibar mheshimiwa, Lela Mohammed Mussa amekabidhiwa rasmi ofisi pamoja na nyaraka za wizara hiyo kuashiria majukumu ya wizara kuachiwa kutoka kwa mtangulizi wake bwana, Mahmoud Thabit Kombo huko katika ukumbi wa wizara hiyo kikwajuni mjini Unguja.

Mara baada ya makabidhiano hayo Lela alisema hana hofu juu ya majukumu yake kutokana na uwepo wa wataalamu mbalimbali pamoja na washauri wenye weledi jambo litakalompa chachu ya kutekeleza majukumu yake na kutimiza malengo ya Serikali ya kuwa na uchumi utakaowanufaisha wananchi wote.

“Wizara ina wataalamu,ina wazoefu wa miaka mingi na ina washauri wazuri hivyo nina imani nikishirikiana na watendaji wenzangu wa kila kitengo tutafanikisha zaidi ya yale tunaoyotarajia” alisema waziri huyo

Alisema ili kuhakikisha malengo yote yanakamilika ikiwa ni pamoja na utekelezaji ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020,dira ya maendeleo pamoja na mpango kazi wa wizara ni wajibu wa kila mtumishi wa wizara hio kuwa anatekeleza majukumu yake kikamilifu bila ya kusimamiwa.

“Ingawa tuna changamoto nyingi ila tuzitumie changamoto hizo kama fursa za kuleta mabadiliko katika jamii” aliongezea Lela

Akizungumzia suala la nafasi za ajira kwa wazawa katika taasisi binafsi zinazofanya biashara za utalii ikiwemo mahoteli na migahawa ya watalii alisema atahakikisha kuona kwamba nafasi hizo zinabakia kwa wazanzibar na aliahidi kuzichukulia hatua taasisi zitakazokwenda kinyume na masharti waliyopangiwa ikiwemo suala la ajira kwa wazawa.

“Tumeahidi ajira laki tatu na utalii una nafasi kubwa katika ajira hizo hivyo wizara ya utalii na mambo ya kale hatutokubali kuona nafasi zipo katika mahoteli ila zinakosekana kutokana na ubabaishaji” alisisitiza 

Mapema waziri mstaafu wa wizara habar,utalii na mambo ya kale  bwana, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba watendaji wa wizara hiyo kutoa mashirikiano kwa waziri mpya ambapo aliahidi kumpa ushauri waziri huyo pale itakapohitajika ili kuona wizara inafikia malengo yaliyokusudiwa.

“ili wizara iweze kufikia malengo ni lazima pawe na mashirikiano hivyo niwaombe kama mulivyokuwa munashirikiana nami na yeye mpeni mashirikiano na mimi milango yangu ipowazi waziri ukitaka ushauri nitakupatia” alisema mstaafu huyo

Makabidhiano hayo yamekuja mara baada ya Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi kutangaza baraza jipya la mawaziri na kumteua muheshimiwa Lela Mohammed Mussa kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *