img

Madiwani waaswa kumuunga mkono JPM

November 26, 2020

Na Timothy Itembe Mara.

MADIWANI wateule waaswa kumuunga mkono Rais awamu ya Tano katika kutenda kazi huku wakitatua matatizo na kero za wananchi waliowachagua.

Kauli hiyo ilitolewa jana na makamu mwenyekiti, mteule,Victoria Mapesa  aliyechaguliwa kwa kupata kura 18 dhidi ya mpinazni wake Deogratius Ndege ambae alipata kura16 dhidi ya kura ziilizopigwa 34.

Mapesa alisema kuwa madiwani waliochaguliwa wanatakiwa kwenda kufanya kazi ya kutatua kero za wananchi huku wakimsaidia Rais John  Pombe Magufli kazi.

“Niwaombe madiwani wenzangu tuliopata ridhaa hii twende tukafanye kazi ya waliotuchagua pamoja na kutatua kero za wananchi huku tukiibua vipaumbele vya miradi katika maeneo yetu pamoja na kumsaidia Mgufuli kazi”alisema Mapesa.

Mapesa aliongeza kusema kuwa kufanya hivyo kutasaida kurahisishia ushindi wa Chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi ambao utafanyika mwaka ili kuwa mwepesi kushinda.

Katika uchaguzi huo mwanamama huyo amekuwa wa kwanza kuchaguliw kama mwenyekiti wa halmashauri hiyo tangu ilipoanzishwa hiyo ikiwa ni matunda ya Taasisi zisizo za kiserikali  kama vile TGNP kushirikiana na serikali iliyopo madarakani kutoa elimu kwa jamii ya kupinga mfumo dume.

Kwa upande wake msimamizi wa uchaguziAbbakari Ghati ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa mkoani Mara alitumia nafasi hiyo kumtangaza  Simion Samwel Kiles kuwa mshindi nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri ya Tarime vijijini ambaye alipata kura 21 kati ya mpinzani wake Godfrey Kegoye aliyepata kura 13 kati ya kura zote zilizopigwa 34

Mwenyekiti huyo mteule alisema akiapishwa atahakikisha anasimamia mapato na matumizi ya fedha za halmashauri kwa lengo la kutekeleza miradi kama ilivyokusudiwa kulingana na fedha zinapokuwa zimetolewa.

Kiles aliongeza kusema kuwa atahakikisha miradi inatekelezwa kila kata bila upendeleo kwa kila diwani kulingana na vipaumbele vya miradi ilivyoibuliwa na wananchi.

 Wakati huohuo aliyechaguliwa kuwa katibu wa madiwani kwa halmashauri ya Tarime vijijini ni Ayubu Marwa na kwa halmashauri ya Tarime Mjini Daniel Komote alichaguliwa kuwa mwenyekiti huku makamu wake aliyechaguliwa ni Thobias Elias Ghati.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *