img

Kansela Merkel awataka Wajerumani kuwa wavumilivu

November 26, 2020

 

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuwa na subra na kuendelea kufuata maagizo yaliyowekwa ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.Merkel amesema leo kuwa kuna matumaini ya kupatikana kwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Akilihutubia bunge hii leo baada ya kukubaliana na wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani juu ya kuongeza muda wa vikwazo hivyo angalau hadi Desemba 20, Merkel amesema serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha maisha yanarudi kama kawaida, lakini pia ina jukumu la kuwalinda watu.

Ujerumani ilitangaza vikwazo vipya mnamo Novemba 2, vilivyolenga kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa COVID-19 kwa kufunga mikahawa, baa, na sehemu za burudani japo ikaamua kuziacha wazi shule, maduka na saluni.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *