img

Jeshi la polisi mkoani Mwanza laagizwa kuwasaka wanaotuhumiwa kuwapa Mimba Wanafunzi

November 26, 2020

Serikali mkoani Mwanza imeliagiza jeshi la Polisi mkoani humo, kuwasaka na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, watu wanaotuhumiwa kuwapa ujauzito zaidi ya wanafunzi 451, katika kipindi cha mwaka 2020.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, ameliagiza jeshi hilo wakati akizindua maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, yaliyoandaliwa na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto (KIVULINI) mkoa wa Mwanza,

Hatua hiyo imefuata kutokana na ongezeko la vitendo vya wanafunzi kukatisha masomo kutokana na ujauzito mkoa wa Mwanza, unaotajwa kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza nchini kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Matukio 1,387 ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, yametokea mkoani Mwanza tangu Januari mwaka huu.

Katika uzinduzi huo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELLA, amesema matukio ya kuwapa ujauzito wanafunzi ni miongoni mwa ukatili ulioshamiri na kutoa maelekezo kwa vyombo vya dola.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza MULIRO JUMANNE, amesema jeshi hilo litaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu ni “TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA MABADILIKO YANAANZA NA MIMI”.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *