img

Diego Maradona: Argentina yaanza maombolezo ya siku tatu, salamu za rambirambi zikiendelea kumiminika

November 26, 2020

Dakika 7 zilizopita

maombolezi

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimeanza nchini Argentina baada ya Maradona kufariki dunia Jumatano akiwa na umri wa miaka 60.

Mwili wake uko katika jimbo la Casa Rosada, moja ya miji muhimu Argentina.

Leo hii hata nyota wa soka kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo “hata hawawezi” kufikiria kupendwa kama ilivyokuwa kwa Diego Maradona. Amesema aliyekuwa mchezaji mwenzake Argentina Ossie Ardiles.

“Haikuwa rahisi kabisa tangu akiwa mdogo kwasababu kipindi hicho pia alikuwa akizungumziwa na vyombo vya habari kila mahali. Hakuwa na maisha ya kawaida kama watoto wengine hata maisha ya ujana wake,” Ardiles amezungumza na BBC.

“Kila mmoja alitaka kuwa naye, kila mmoja alitaka kuzungumza naye.” Ameongeza.

Maradona, ambaye alichezea vilabu ikiwemo Barcelona na Napoli, alikuwa nahodha wa timu ya Argentina na alishinda kombe la dunia mwaka 1986 na kufunga bao la kihistoria lililofahamika kama ‘Hand of God’ dhidi ya England katika robo fainali.

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Tottenham Ardiles, aliyecheza pamoja na Maradona katika kombe la dunia mwaka 1982, anasema alikuwa kama “miungu” nchini Argentina, Naples na kote duniani.

m

Mwili wa Maradona utafanyiwa uchunguzi hii leo.

Maradona aliyekuwa mshambuliaji kiungo wa kati na kocha wa Argentina, mapema Novemba alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo na alikuwa anasubiri kupata matibabu ya kucha kutegemea pombe.

Katika mechi za Mabingwa Jumatano, watu wote uwanjani walikaa kimya kwa dakika moja kutoa heshima zao za mwisho, tukio ambalo linatarajiwa kutokea kabla ya kuanza kwa mechi zingine zote za Ulaya wiki hii.

Wengine wanaotoa rambirambi zao

Messi na Ronaldo ni miongoni mwa wachezaji waliotoa rambirambi zao, huku mchezaji wa Brazil Pele akisema alitarajia iko siku “wangecheza pamoja mpira”.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema Maradona “alifanya mpira kuwa bora”.

“Kulikuwa na bango Argentina, mwaka mmoja uliopita, nililosoma ambalo lilikuwa limeandikwa: haijalishi ulichokifanya katika maisha yako, Diego, muhimu ni kile ulichofanya katika maisha yetu,’” aliyekuwa kocha wa Barcelona na Bayern Munich Guardiola aliongeza.

m

Pia ametuma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kwa niaba ya Manchester City

Aliyekuwa mshambuliaji wa Scotland Frank McGarvey alikuwa timu ya upinzani pale Maradona akiwa na umri wa miaka 18 na kufunga bao lake la kwanza kwa Argentina, katika mechi ya kirafiki uwanja wa Hampden mwaka 1979.

McGarvey anasema ni wazi Maradona tayari mchezo wake ulikuwa wa kiwango kingine wakati huo.

“Niliambiwa nimtazame kijana huyu ambaye mchezo wake ulikuwa mzuri,” McGarvey amezungumza na Shirika la habari la Press Association. “Alikuwa kijana mdogo lakini haungeamini macho yako. Alitufanya tuwe kama wasiojielewa. Alikuwa na kasi zaidi ya mara tano na pia kasi ya kukuondokea uwanjani.

“Nakumbuka nikimkimbiza. Nilikuwa ninamkimbiza haswa akiwa ameshika mpira na ananiondokea, nikamuachia David Narey na Paul Hegarty na kuamua kumkaba koo mchezaji mwingine. Alikuwa mzuri kunishinda. Alicheza vizuri kwa njia zote.

“Messi na Ronaldo ni wachezaji wazuri lakini hawaingii kwa Maradona, mchezo wake ni bora kuliko wote. Ni siku ya huzuni sana kwangu. Ni mchezaji mzuri ambaye sijawahi kumuonea mwenzake.”

Mchezaji Harry Kane aliweka picha mtandaoni inayomuonesha yeye akiwa na Maradona huku Marcus Rashford akimuelezea mchezaji huyo kama “legendary”.

h

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *