img

Azam FC yamfuta kazi kocha wake Aristica Cioaba

November 26, 2020

Kocha Aristica Cioaba amefutwa jumlajumla kazi ndani ya Azam FC msimu wa 2020/21 kutokana na matokeo mabaya aliyopata hivi karibuni.

Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari Zakaria Thabit umesema kuwa mchakato umefanyika kuanzia timu ilipopoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na mechi zilizofuata timu ilicheza chini ya kiwango.

“Timu imekuwa ikicheza chini ya kiwango baada ya kupoteza mbele ya Mtibwa Sugar, hata tuliposhinda mbele ya Dodoma Jiji bado hakukuwa na kiwango bora.

“Kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Yanga hali ilikuwa hivyo na tumepoteza hivyo makubaliano ya pande zote mbili tumefika makubaliano na kwa sasa Vivier Bahati atakuwa Kaimu Kocha Mkuu,” amesema. 

Cioaba amesimamia Kwenye mechi 12 amepata ushindi mechi 8 sare moja kichapo 3.

Vipigo viwili mfululizo ilikuwa mbele ya KMC na Yanga kwa kufungwa bao mojamoja.

Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 18 na ile ya ulinzi imefungwa mabao sita.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *