img

Waziri wa mawasiliano achagua kikosi kazi

November 25, 2020

Na Thabit Madai, Zanzibar.

WAZIRI  wa Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali ameunda Timu ya Wanasheria sita kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakayofuatilia mikataba yote iliyomo katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vilivyopo Zanzibar.

Kamati hiyo imeundwa kutokana na  agizo la Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdallah alilolitoa kwa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi kutokana na changamoto alizozingundua wakati wa ziara yake.

Hayo ameyasema leo katika hafla ya kuzindua wa kamati ya  Wanasheria iliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi uliopo Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Amesema kamati hiyo ya wanasheria  iliyoundwa itahakikisha  inafuatilia na kuipitia upya mikataba iliyopo chini ya viwanya ya ndege ili  kubaini changamoto zinazoikabili Mamlaka hizo.

Akiitaja mikataba hiyo iliyotiwa saini ni pamoja na mikataba ya wafanyakazi, miradi iliyoanzishwa kwenye viwanja hivyo kwa lengo la kuhakikisha mapato yanayokusanywa kwenye huduma za jamii yanasimamiwa na kukidhi mahitaji halisi kwa maendeleo ya Zanzibar.

“Ikachunguzwe Mikataba yote na tufichue changamoto zote zilizomo kwenye mikataba hiyo, tuache kuoneana muhali kwani tumewapa kazi hii kwa kuwaamini na tunatarajia mafanikio mazuri kutoka kwenu. ” alisema Waziri huyo. 

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mustafa Aboud Jumbe aliisisitiza Kamati hiyo kufanya kazi bila ya kuingiliwa na mtu yeyote na kuweza kuhoji na kudai nyaraka ambazo zitakazowasaidia katika kukamilisha majukumu waliyopewa na Waziri huyo.

Nao Wajumbe wa kamati hiyo wameahidi kuifanya kazi hiyo bila ya kumuonea muhali mtu au taasisi kwa maslahi na maendeleo ya Taifa.

Kamati hiyo imepewa siku tano (5) za kufanya kazi na mara tu watakapomaliza  kazi yao watawasilisha kwa Waziri huyo ili aweze kuendelea na hatua nyengine.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *