img

Waziri mkuu wa Ethiopia ataka jumuiya ya kimataifa isiingilieamzozo wa Tigray

November 25, 2020

 

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameiambia jumuiya ya kimataifa isiingilie mzozo wa jimbo la Tigray, katika kipindi hiki ambacho muda wa mwisho wa masaa 72 aliowapa waasi katika jimbo hilo wajisalimishe ukifikia ukingoni. 

Katika taarifa yake kiongozi huyo amesema Ethiopia kama taifa huru lina haki zote kusimamia sheria zake na kuzitekeleza ndani ya mipaka yake. 

Licha ya kauli yake hiyo laikini, ujumbe wa Umoja wa Afrika unaowajumuisha marais watatu wa zamani unaelekea mjini Addis Ababa katika juhudi za usuluhishi. Hao ni rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, rais wa zamani wa Msumbiji Joachim Chisano, na Kgalema Motlanthe aliyekuwa rais wa mpito wa Afrika Kusini. 

Wakati huo huo, Jake Sullivan aliyeteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais mteule wa Marekani Joe Biden, amejiunga na wanaotoa miito ya kuhimiza mazungumzo kuumaliza mzozo huo wa Tigray.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *