img

Wafanyakazi Wizara ya nchi ofisi ya Rais watakiwa kutumia elimu walizonazo kuleta mabadiliko ya kimaendeleo

November 25, 2020

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali amewataka Wafanyakazi wa Wizara hiyo kutumia elimu walizonazo kwa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika Ofisi hiyo na Taifa kwa Ujumla.

Amesema Wizara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya Wananchi hivyo ni vyema Wataalamu wa fani mbalimbali waliomo kuwa Wazalendo na kuhakikisha wanafikia malengo ya Serikali ya awamu ya nane ya kufikia uchumi wa Bluu.

Waziri Jamal ameyasema hayo huko Ofisini kwake Vuga wakati wa makabidhiano ya Ofisi na Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa aliemaliza muda wake.

Amesema Timu ya Uongozi aliokabidhiwa ni nzuri kwani inawataalamu wengi na wa fani mbalimbali na kuahidi kuendeleza mwendo wa kasi katika kuleta maendeleo.

Aidha amepongeza Waziri huyo mstaafu kutokana na kazi na jitihada kubwa alizozichukuwa katika Uongozi wake na kuacha msingi mkubwa kwa faida ya Wizara na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri Mstaafu wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia amesema maendeleo yaliyopatikana yametokana na Ushirikiano wa Wafanyakazi wa Wizara hiyo hivyo ni muhimu kutoa ushirikiano na Waziri mpya ili kuweza kuyaendeleza na kufanya kazi kwa ufanisi.

Aidha amewakumbusha Wafanyakazi hao kufanya kazi kwa Uzalendo na kutosahau kuwa wanatakiwa kuwa Waaminifu na kukinai katika uwajibikaji wa kazi zao.

Nao Wafanyakazi wa Wizara ya nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wamemshukuru Waziri aliemaliza muda wake kwa ushirikiano aliowapa na kuahidi kushirikiana na Waziri mpya kwa maslahi mapana ya Wananchi wa Zanzibar.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *