img

Wabunge wa Libya wakutana Morocco kuliunganisha bunge lililogawika

November 25, 2020

Wabunge kadhaa kutoka pande zote za kisiasa katika nchi iliyoharabiwa na vita ya Libya, walikusanyika nchini Morocco kushiriki katika mazungumzo ya kuutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo. 

Bunge la Libya limegawika katika makundi mawili, kundi moja likiwa katika mji mkuu wa Tripoli na kundi jingine lipo katika mji wa mashariki wa Tobruk. 

Mikutano hiyo inafanyika wakati wajumbe wa Libya wakirejea katika mazungumzo tofauti yanayoongozwa na Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kuhusu mfumo wa uteuzi wa baraza kuu la kuiondoa nchi hiyo kwenye mgogoro na kuitayarisha kwa uchaguzi. 

Baraza la Wawakilishi, ambalo limekataa kuidhinisha serikali ya Tripoli, lina mpasuko mkubwa wa ndani. Mikutano hiyo iliyoandaliwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi imepongezwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya – UNSMIL.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *