img

Vital Kamerhe: Mshirika wa rais DRC yuko hoi gerezani

November 25, 2020

Dakika 10 zilizopita

Vital

Waziri wa sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ameonya kuhusu hali ya afya ya Vital Kamerhe, msimamizi wa wafanyakazi wa rais Felix Tshikedi ambae, alihukumia kifungo cha miaka ishirini jela tangu mwezi Juni.

Kamerhe alikutwa na hatia ya kupora zaidi ya dola milioni hamsini za kimarekani ambazo Felix alitoa kwa ajili ya mpango wake wa siku mia moja madarakani.

Lakini hadi sasa Vital Kamerhe na chama chake wameendelea kutupilia mbali tuhuma hizo wakikosao baadhi ya wanachama cha rais Felix Tshisekedi kumzuia Vital Kamerhe asigombee katika uchguzi wa mwaka2023 kama walivyokubaliana katika uchaguzi wa mwaka 2018.

Ni miezi tatu sasa tangu Vital Kamerhe alazwe hospitalini katika hospitali moja mjini Kinshasa.

Chama chake kiliomba mara kadhaa kuwa serikali imuhamishe hospitali au impeleke nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi lakini waziri wa sheria hakukubali maombi hayo.

Ingawa hapo jana waziri wa sheria alienda kujionea mwenyewe hali ya afya ya mshirika huyu wa karibu wa rais Felix Tshisekedi ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka ishrini gerezani.

Kwa mujibu wa waziri wa sheria Bernard Takahishe amesema hali ya afya ya mwanasiasa huyo maarufu inchini humo iko hatarini.

“Nilienda kumuangalia bwana Vital Kamerhe, kweli hali yake ya kiafya ni mbaya Sana,anapaswa kupata matibabu mazuri.

Ikibidi kuomba asafirishwe nje ya nchi tutajadiliana na idara za huduma ya afya ili tupange pamoja. Lakini kwa sasa tunafuatilia kwanza apate matibabu hapa inchini lakini tukiona kama hakuna mabadiliko basi tutampeleka nje.”

drc

Kwa mujibu wa Aimé Boji katibu mkuu wa chama UNC cha Vital Kamerhe , amesema kuona kitendo cha waziri wa sheria kutembelea mfungwa huyu inawapa moyo na kuona

kuwa anaweza kupata tiba sahihi kuokoa maisha yake.

“Raia wengi hapa nchini DRC wanahofia juu ya afya ya Vital , Christ Lyda anasema.

Na kuna hofu kuwa Kamerehe anaweza kukwepa kifungo chake ikiwa atasafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

“Tunajua vizuri wanasiasa wetu, wanalalamika kuwa wadhaifu zaidi kila mara wakiwa jela na hiyo yaweza kuwa njama ya kisiasa ili wamtoroshe bwana Viltal Kamerehe.

Kama mimi niliwahi kuzuilizwa jela na huko ndani kuna hospitali, lazima apewa matibabu ndani ya hospitali ya gereza kubwa kama sivyo basi.

Watafute hospitali nyingine kubwa hapa suala la kumusafirisha nje ya nchi mimi binafsi siwezi kukubali kwa kuwa mwanasiasa huyu aliiba pesa nyingi za nchi”

Kwa mujibu wa Aimé Boji katibu mkuu wa chama cha Vital Kamerehe, wale wanaofikiria hivyo hawajuwi kuwa suala la afya ya mtu sio jambo la kufanyia masihala.

“Nimewaambia Wakomamani wote wanaohisi kama Vital anaweza toroka kama, waachane na mtazamo huo.

Ni muda murefu sasa tualianza kuwaambia viongozi kuwa mkuu wa chama chetu amedhoofika kiafya na waziri wa sheria yeye mwenyewe aliona Vital yupo kwenye hali gani, sasa kwanini tudanganye, sisi

tumeomba apewe matibabu mazuri hata hapa nchini.”

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *