img

Uchaguzi wa Marekani 2020: Je kukabidhiana madaraka ya urais ni nini?

November 25, 2020

Dakika 6 zilizopita

President-elect Joe Biden

Rais Trump bado hajakubali kushindwa na Joe Biden lakini amekubali mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka kuanza, huku wanasheria wake wakiendelea na makabaliano ya kisheria.

Je mchakato huo unahusisha nini na kwanini ni muhimu?

Section divider

Kukabidhi madaraka ni nini?

Ni mpango wa kumpokezana majukumu kama vile taarifa muhimu kati ya utawala ulioko madarakani na ule unaoingia madarakani- kuhakikisha rais mteule na timu yake wanafahamu kila kitu kinachoendelea kabla ya kuingia ikulu ya White House.

Utawala unaoingia madarakani unasaidiwa shirika linayaloshughulikia mabadilishano hayo linalofahamika kama General Services Administration (GSA), ambalo linatoa fedha na usaidizi wa vitu kama nafasi ya ofisi, vifaa na teknolojia.

Mchakato huo ambao unadumu kwa karibu wiki 11, kuanzia pale ambapo mshindi wa uchaguzi wa urais anapobainika, hadi Januari 20 wakati rais mwingine anapoingia rasmi madarakani.

Sio kazi moja pekee inayopokezwa – rais mpya anatakiwa kujaza nafasi za uteuzi wa kisiasa karibu 4,000, kwa mujibu wa kituo cha urais cha kukabidhi madaraka.

Section divider

Nini kinafanyika wakati huo?

Kuna mambo matatu makuu hufanyika – wafanyakazi, kupokea maelezo, na kupanga ratiba ya kazi ya rais mteule.

Wakati mchakato wa kukabidhi madaraka unapoanza rasmi, mipango ya kazi inaendeshwa na timu ya rais mteule ambayo imekuwa ikijiandaa wakati wote wa kampeni.

Moja ya masuala muhimu ni matano ya kila siku wa usalama.

Wagombea wote wa kiti cha urais hupokea baadhi ya maelezo kuhusu usalama wa kitaifa kabla ya uchaguzi, lakini maelezo hayo hayatolewi kila wakati na kwa undani kama zile anazopewa rais mteule.

Bwana Biden sasa atapokea maelezo ya kila siku ambayo yameorodheshwa kuwa taarifa za siri, kuhakikisha utawala mpya unajiandaa endapo chochote kitatokea.

Presidents Clinton and George W Bush inside the White House

Tume ya uchunguzi wa shambulio la Septemba 11 lililofanyika mwaka 2001 ilibaini kuwa kuchelewa kwa mchakato wa kukabidhiana madaraka baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 huenda kulichangia utawala wa Bush wakati huo kushindwa kuzuia shambulio hilo.

Utawala mpya unaoingia madarakani pia unaongezewa ofisi ya ziada na viti, inapojiandaa kwanza katika ikulu ya White House.

Mikutano ya kawaida hupangwa na maafisa wa serikali ya sasa kusaidia katika mpango wa wafanyakazi na mabadiliko ya sera, na wakati huo wafanyakazi wa muhimu wa utawala mpya watakuwa wanafanya kazi chini ya wenzao wanaoondika wanapojiandaa kuanza majukumu yao mapya.

Bwana Biden tayari ameanza kuwateua watumishi wake, lakini mchakato wa kupokezana madaraka unasaidia wakuu wa kila idara ya serikali kujua ni nafasi zipi zinastahili kujazwa.

Kati ya nyadhifa 4,000 za kisiasa ambazo zinajazwa na utawala mpya unaoingia madarakani, karibu 1,200 zinahitajika kuidhinishwa na seneti- huku serikali ikisaidia kutoa maelezo kuwahusu kipindi hicho cha mpito.

Mwaka huu, kutokana na janga la corona, Bwana Biden amesema anataka kushirikiana zaidi na mashirika ya afya na maafisa wa ngazi ya juu wa afya ili kupata maelezo kamili kuhusu afya ya umma .

Joe Biden

Pia amekuwa akikutana na maafisa wa serikali,na kamati ya mpito ya kwa ushirikiano na Wizara ya mambo ya nje hupanga mawasiliano ya simu kati ya rais mteule na viongozi wa kimataifa.

Timu ya Bwana Biden imekuwa ikiwasiliana kupitia njia ambazo sio rasmi. Lakini sasa itaweza kutumia barua pepe rasmi ya serikali na kufikia mifumu ya usalama.

Kuambatana na chaguzi zilizopita, rais mteule na mke wake huwa wanatembezwa katika Ikulu ya White House na kuombwa wachague rangi wanazopenda na muonekano wa makazi yao mapya kabla wayahamie – lakini hatua hiyo sio masharti ya kisheria.

Section divider

Kwanini mchakato huu wa ulichekeweshwa?

Huwa unatakiwa kuanza mara baada shirika la GSA kuandika barua ya kumtambua rais mteule anayeingia madarakani .

Lakini mwaka huu, shirika la GSA halikuandika barua ya kumtambua Bwana Biden kama mshindi hadi tarehe 23 mwezi Novemba – karibu wiki tatu baada ya uchaguzi kufanyika.

Ground upwards view of front of GSA building

Hatua hiyo iliizuia timu ya Biden kupata fedha na usaidizi mwingine

Kisheria mchakato haujawekwa wazi unatakiwa kuanza lini, ikizingatiwa kuwa utawala wa Trump unatumia mwanya huo kuchelewesha mpango huo kwasababu unapinga matokeo ya uchaguzi.

Chini ya katiba ya ya Marekani, GSA ina wajibu wa kuidhinisha mchakato huo mara tu baada ya “mshindi mtarajiwa” kujulikana, japo hakuna tarehe rasmi ya iliyotengwa ni lini hatua hiyo ifanyike.

Ishawahi kucheleweshwa – mwaka 2000 mchakato wa kukabidi madaraka ulicheleweshwa kwa muda baada ya matokeo ya uchaguzi kupingwa mahakamani, lakini ushindani katika uchaguzi huo ulikuwa mkubwa kuliko wa mwaka huu.

Hali ya sasa ni tofauti ikilinganishwa na wakati wa Bwana Trump ambaye ushindi wake ulitambuliwa na GSA siku moja baada ya uchaguzi wa mwaka 2016 – hata kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa rasmi – na alikutana na Rais Barak Obama katika ikulu ya White House siku iliyofuata.

Section divider

Nani anagharamia mchakato huu?

Mchakato huu unagharamiwa na kupitia mkusanyiko wa fedha za serikali na fedha za kibinafsi.

Punde rais mteule anapotambuliwa na GSA, karibu dola milioni saba za serikali kuu hupewa utawala mpya unaojiandaa kuingia madarakani.

Fedha hiyo baadae huongezwa na rais mteule.

Gazeti la New York Times liliripoti kuwa Bwana Biden alitenga karibu dola milioni saba zitakazotumika kufadhili mpango wake wa kuingia madarakani mapema mwezi Novemba, na pia ameomba fedha zaidi kutoka kwa wafuasi wake.

Fedha hilo zote zinatumiwa kulipa mamilioni ya dola zinazotumika kugharamia mchakato huo wa kupokezana mamlaka ya urais.

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *