img

RC Malima Aunda Kamati Kuchunguza Kuungua Bweni

November 25, 2020

MKUU wa mkoa wa Mara, Adam Malima, ameunda kamati kwa ajili ya kuchunguza moto ulioteketeza bweni la wavulana la shule ya Sekondari Bumangi iliyopo wilayani Butiama ambapo kamati hiyo itaongozwa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Augustine Magere ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

 

Bweni hilo liliteketea Novemba 23, majira ya saa moja usiku wakati wanafunzi wakiwa kwenye vipindi vya dini na kuteketeza kila kitu huku kukiwa hakuna tukio la majeruhi wala vifo.

“Tukio la moto katika bweni la shule ya Sekondari Bumangi, limezua utata na maswali mengi kutokana na ukweli kuwa bweni hilo lilifungwa saa 12.50 jioni ili wanafunzi waweze kwenda darasani kwa ajili ya vipindi vya dini kabla ya kuanza masomo ya usiku saa 1.30.

“Niwaombe wadau mbalimbali kuwasaidia watoto hawa, maana nguo walizonazo kwa sasa ndizo walizobaki nazo, atakayeguswa atushike mkono kwenye hili lakini pia watusaidie magodoro na mashuka  na madaftari, maana kila kitu kimeteketea.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa katika tukio la kuungua moto kwa bweni katika Shule ya Sekondari Bumangi hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa  ingawa bweni hilo limeteketea kabisa sambamba na samani zilizokuwemo na mali za wanafunzi,” amesema Malima.

 

The post RC Malima Aunda Kamati Kuchunguza Kuungua Bweni appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *