img

Rapper AKA na mpenzi wake wakamatwa na polisi

November 25, 2020

 

Rapper toka Afrika Kusini, Kiernan Jarryd Forbes maarufu #AKA na mpenzi wake #NelliTembe wajikuta Kituo Cha Polisi Baada ya kuingia kwenye mabishano yaliyotokana na uvumi wa kuchepuka kati yao. Imeelezwa.

Kupitia mitandao ya burudani nchini humo, imeeleza kuwa wapenzi hao waliingia kwenye malumbano makali kiasi cha majirani kuita mapolisi, ambapo mapolisi walipofika eneo la tukio walilazimika kuingilia kati na mrembo #Nelli alinukuliwa akitaka kuvunja Mahusiano yake na AKA.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, mrembo #NelliTembe alieleza kuchoshwa na tabia zinazohusishwa na uvumi wa hali ya #AKA kutokuwa muminifu ambapo siku ya malumbano hayo alikuwa ameshafungasha vitu vyake tayari kundoka nyumbani kwa Rapper huyo.

Malumbano yalipopamba moto zaidi kati ya Nelli na AKA ambapo maafisa polisi walifikia maamuzi ya kuongozana nao hadi kituo cha polisi cha Randburg.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *