img

Rais Kenyatta azindua mchakato rasmi wa mbadiliko ya katiba

November 25, 2020

Dakika 6 zilizopita

Uhuru

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amezindua rasmi mpango maalum wa kukusanya saini zitakazo anzisha mchakato wa kura ya maoni ili kufanyia marekebisho katiba.

Kinyume na ahadi ya Rais Uhuru Kenyatta kuwa mchakato huo ni wa kuunganisha wakenya wote, Naibu wa Rais William Ruto na baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono walisusia zoezi hilo.

Juhudi za Bwana Ruto za kupinga mageuzi ya katiba, kama inavyopendekezwa na rais Uhuru Kenya na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga, zinaonekana kugonga mwamba baada ya Rais kenyatta kuzindua rasmi mchakato wa kukusanya sahihi ili kuidhinisha kura ya maoni ya kubadili katiba.

Ruto ambaye amekuwa mkosoaji wa mchakato huo wa kufanya mageuzi ya kikataba hakuhuduria hafla hiyo sawa na wabunge wanaomuunga mkono ambao wote wamedai kuwa zoezi la kubadili katiba sio suala la dharura na badala yake fedha ambazo zitatumika katika mpango huo kutumiwa kukabiliana na janga la corona na kufadhili miradi ya maendeleo ili kupunguza viwango vya umaskini.

Lakini akiongea wakati wa hafla hiyo Rais Kenyatta alisema mpango huo wa kubadilisha katiba unadhamiria kumaliza mizozo ya kisiasa ambayo imeshuhudiwa nchini kenya kila baada ya uchaguzi mkuu.

bbi

Kuhusu tangazo la mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai George Kinoti kuwa ameanzisha uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008, Bwana Kenyatta ameshutumu hatua hiyo akisema hatakubali vitendo ambavyo vitafungua kile alichokitaja vidonda vya zamani na kuwaonya wale ambao wanataka kutumia machufuko yaliyofanyika kipindi cha nyuma kuzua uhasama na hali ya wasiwasi.

Hata hivyo wakenya wengi wanasema kuwa licha ya rais Uhuru Kenyatta kushinikiza kuidhinishwa kwa katiba mpya, wao hawajapokea nakala ya rasimu hiyo ya katiba au hawafahamu yaliyomo kwenye mapendekezo mapya.

Shughuli ya kukusanya saini hizo itaendelea kwa muda wa wiki moja kabla ya kuwasilisha kwa tume ya uchaguzi.

Huwezi kusikiliza tena

Maelezo ya sauti,

Je ripoti ya BBI ndio suluhisho la amani na umoja wa kudumu Kenya

Source link

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *