img

Ndege za kivita za Israel zashambulia maeneo ya kusini mwa Syria

November 25, 2020

Shirika la habari la Syria SANA, limedai kuwa ndege za kivita za Israel jana jioni zilifanya mashambulizi yaliyolenga maeneo kadha ya kusini mwa Syria. 

Shirika hilo limenukuu taarifa kutoka chanzo kimoja ndani ya jeshi, ikisema kuwa mashambulizi ya Israel yalitokea katika maeneo yanayokaliwa ya Golan kuelekea kusini mwa mji wa Damascus. 

Wiki iliyopita, ndege za kivita za Israel ziliyashambulia maeneo tofauti ya Syria. Kwa mujibu wa vyanzo ndani ya Syria, askari watatu waliuawa wakati wa mashambulizi hayo.

 Shirika la haki za binadamu la Syria limedai kuwa tangu mwaka huu uanze, Israel imefanya mashambulizi 35 dhidi ya maeneo tofauti ya Syria na kuwaua watu 198. 

Mashambulizi ya Israel yanaoneka kama jaribio la kuizuia Iran, mmoja wa washirika muhimu wa rais Bashar al-Assad, kupanua ushawishi wake wa kijeshi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *