img

Mwamnyeto Amfunika Maguire

November 25, 2020

BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga ya Bongo amemfunika jumlajumla beki wa kati ya Klabu ya Manchester United, Harry Maguire katika kuweka lango lake salama kwenye mechi za ligi ambazo wamezicheza.

 

Kwa Bongo, Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 11, Mwamnyeto ameanza kikosi cha kwanza mechi 10 ambazo ni dakika 900 huku safu yake ya ulinzi ikiruhusu mabao manne. Maguire ameanza kikosi cha kwanza England mechi nane ambazo ni dakika 720 na timu yake imeruhusu mabao 13.

 

Mwamnyeto amekuwa na wastani wa kuokota bao moja kwenye nyavu kila baada ya dakika 225 licha ya kucheza mechi nyingi huku Maguire akiwa na wastani wa kuokota bao moja kila baada ya dakika 53.

 

Ingizo jipya la Yanga kutoka Coastal Union ndani ya dakika 900, ameonyeshwa kadi moja ya njano ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Namungo baada ya kumchezea faulo, Shiza Kichuya na kusababisha penalti moja huku Maguire ingizo jipya kutoka Leicester City ana jumla ya kadi mbili za njano.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

The post Mwamnyeto Amfunika Maguire appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *