img

Mkali Wenu: Alikiba Aliniomba Kumuandikia Mediocre

November 25, 2020

Mchekeshaji Mkali Wenu ametoa kali ya mwaka baada ya kufunguka kumuandikia wimbo wa mediocre ya msanii Alikiba ambapo amesema awali wimbo huo alitaka ampatie Nay wa Mitego ila aliishindwa.

 

“Kitu chochote kinaweza kutokea, kama menejmenti yangu ikisema nifanye kazi na Alikiba nitafanya naye, kwa sababu Alikiba ni mshkaji wangu na namuandikia nyimbo, hata hii nyimbo aliyotoa ya mediocre nilikuwa nayo muda mrefu aliniomba nikamuandikia, ukiangalia ina utofauti na nyimbo zake zingine,” amesema Mkali Wenu.

 

“Kumuandikia mtu haimaanishi kama hauna sauti ila Alikiba yeye ana sauti nzuri, mimi nina sauti ila sio nzuri kwenye kuimba, nyimbo ya mediocre imekaa vizuri kwake nilishawahi kumpa Nay wa Mitego akasema haiwezi kuiimba…”

 

Aidha, Mkali Wenu amesema ‘role model’ wake alikuwa ni marehemu Sharo Milionea ambaye alianzia kwenye uchekeshaji kisha kuimba hivyo wasishangae kumuona na yeye akianza kuimba.

The post Mkali Wenu: Alikiba Aliniomba Kumuandikia Mediocre appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *