img

Mavituz ya Carlos Carlinhos Canatisha

November 25, 2020

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, ametaja sifa tatu alizonazo kiungo wake mshambuliaji, Carlos Fernandez ‘Carlinhos’.

 

 

Carlinhos mwenye mavituz ya kutisha uwanjani, Jumapili alianza katika kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Namungo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili na nusu akiuguza maumivu ya kisigino.

 

Staa huyo mpya ndani ya Yanga, amefanikiwa kufunga mabao mawili, huku akipiga asisti mbili, zote zilitokana na mipira ya kona ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze aliitaja sifa ya kwanza aliyonayo Carlinhos ni kupiga pasi fupi na ndefu zinazofi ka kwa usahihi kwa wenzake.

 

Kaze aliitaja sifa ya pili ni uwepo wa ndani ya 18 muda wote wakati timu ikishambulia na kubainisha kwamba hiyo ndiyo sababu ya yeye kumuanzisha juzi katika mchezo dhidi ya Namungo FC na kufanikiwa kufunga bao la kuongoza kabla wapinzani hawajasawazisha.

 

Aliitaja sifa nyingine ya tatu ni uwezo wake wa kupiga mipira ya faulo na kona ambayo mingi anayoipiga mazoezini na kwenye mechi imeonekana kuzaa matunda.

 

“Mara nyingi nimekuwa nikimzungumzia Carlinhos, ukweli ni mchezaji wa kipekee mwenye faida kwenye timu ambaye uwepo wake uwanjani unaipa matokeo mazuri timu.

 

“Carlinhos anaweza asionekane uwanjani muda mrefu, lakini akija kuonekana basi anafanya kitu kimoja kizuri chenye faida kwenye timu, hivyo anastahili kuwepo katika kikosi changu,” alisema Kaze.

 

Kaze aliongeza kuwa, kijana wake huyo huwa anafanya vitu vingi kwa usahihi vile anavyomuelekeza anapokuwa mazoezini ambapo huvihamishia uwanjani jambo ambalo lina faida kwa timu yake.

The post Mavituz ya Carlos Carlinhos Canatisha appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *