img

Mara ; Kijana atishia kumuuwa Mama yake Mzazi

November 25, 2020

Mama mwenye umri wa miaka 54, Mariam Josia, mkazi wa Kitongoji cha Kiabakari kijiji cha Nyambuli wilayai Serengeti mkoani Mara, amesema amekuwa akitishiwa kuuawa na mtoto wake wa kiume aitwaye Juma Mkami.

Akiongea na East Africa Television, Bi. Mariam Josia amesema amekuwa akinyanyaswa na kupewa vitisho na mtoto wake huyo, chanzo kikiwa ni mgogoro wa ardhi baina yake na kijana huyo.

Aidha amesema kijana Juma Mkami amekuwa akishirikiana na mjomba wake kudai kutaka kumiliki ardhi hiyo ambayo ni mali ya urithi. Pia amemtuhumu Mtendaji wa kijiji cha Nyamburi aitwaye Jeremia Gitaro  kuwa chanzo cha kukuwa kwa mgogoro huo wa kifamilia.

Mariam Josia amesema , mumewe alimtelekeza miaka mingi akaishi na watoto wake, lakini anashanga kwa sasa kijana wake mkubwa kuanza kumfanyia vitendo vya kikatili na kulazimisha kupewa sehemu ya ardhi kwa ajili ya kuishi na familia yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiabakari Joseph Mwikwabe, amesema kuwa mgogoro huo wa kifamilia ni wa muda mrefu na kuomba viongozi wa juu kulitatua suala hilo, kwani linaweza kuleta maafa baina ya mama na mtoto wake.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *