img

Kijana wa Miaka 24 Agombea Urais Uganda

November 25, 2020

KIJANA John Katumba ameandika historia nchini Uganda  kuwa  mgombea urais  binafsi mwenye umri mdogo akiwa na miaka 24.

Katumba alizaliwa  Nsabwe wilayani Mukoko na   taarifa zinabainisha kuwa, wazazi wake walifariki akiwa na miaka miwili.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume ya Uchaguzi nchini humo, hakuna kijana kama yeye aliyewania urais katika historia ya Uganda ambaye ameweza kugombea baada ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2018 ambayo yaliondoa kigezo cha umri wa kugombea urais.

Katiba ya Uganda kifungu cha 102b kabla ya mwaka 2018 kiliweka wazi kuwa mgombea urais alipaswa kuwa na umri wa miaka 35 hadi 75.

Katumba ameahidi kujenga viwanja vya ndege vya kisasa, kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kuboresha huduma za jamii, kuzalisha ajira kwa vijana na kusimamia uhuru wa kujieleza.

The post Kijana wa Miaka 24 Agombea Urais Uganda appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *