img

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Ethiopia kuwalinda raia Tigray

November 25, 2020

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anahoia hali ya raia jimboni TigrayImage caption: Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anahoia hali ya raia jimboni Tigray

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ana “hofu kubwa” kuhusu hali ya watu wa jimbo la Ethiopia la Tigray na anaunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika za kutuliza hali katika eneo hilo, Msemaji wa Umoja wa mataifa, Stephane Dujarric amesema.

Bw Guterres pia ametoa wito wa ulinzi wa raia kabla ya tisho la jeshi la Ethiopia la kuanza mashambulio dhidi ya mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.

“Tunafuatilia ripoti za uwezekano wa hatua ya kijeshi kwa hofu kubwa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ana hofu kubwa kuhusu athari zitakazosababishwa na mashambulio hayo kwa raia, kuhusu uwezo wetu wa kusambaza misaada ya kiutu katika eneo ambalo ni vigumu kufanya hivyo .” Bw Dujarric amesema.

“Amewataka viongozi wa Ethiopia kufanya kila liwezekanalo kuwalinda raia, kuzingatia haki za binadamu, na kuhakikishamisaada ya kibinadamu inaweza kusambazwa kwa watu wanaoihitaji.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *