img

Kamugisha Mwenyekiti mpya Halmashauri ya Chalinze

November 25, 2020

Na Omary Mngindo, Chalinze.

GODFREY Kamugisha diwani mpya kutoka Kata ya Ubena, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Katika uchaguzi huo wa kupatikana kwa viongozi hao, Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Ismail Msumi, diwani Kata ya Kimange, ambapo Kamugisha ataiongoza kwa miaka motano ijayo, wakati Makamu nafasi inayopigiwa kura kila mwaka.

Kwenye uchaguzi huo Kamugisha aliwashinda wagombea wenzake Jackson Mkango diwani Kata Pera na Selestine Semiono Msata ambapo Kamugisha alipata kura 12 Semiono 8 wakati Mkango akipata kura 2.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Kamugisha alisema kuwa madiwani wamekabidhiwa jukumu la kuwaongoza wana-Chalinze, hivyo kumalizika kwa uchaguzi Oktoba 28 na la Uenyekiri wa Halmashauri, kwa umoja wao washirikiane kuwatumikia wananchi.

“Tumetoka katika uchaguzi wa Uenyekiti wa Halmashauri yetu ya Chalinze, nitumie nafasi hii kuwashukuru madiwani wenzangu kwa kuonesha imani yao kwangu, hapa hakuna mshindi isipokuwa katika mchakato wetu alitakuwa mmoja,” alisema Kamugisha.

Aliongeza kuwa kwa umoja wao watashirikiana kusogeza mbele maendeleo yaliyopatikana kupitia uongozi uliomaliza muda wake, huku akionesha matumaini makubwa kutoka kwa madiwani wenzake kwamba kwa umoja wao watafanyakazi ipasavyo.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Kibindu Ramadhani Mkufya alisema kwa umoja wao wamedhamiria kutekeleza kazi zao kwa umoja wao ili kuwapatia maendelea wana-Chalinze, huku akieleza kwamba madiwani wote wa natokea Chama Cha Mapinduzi.

“Madiwani tuna morali wa hali ya juu, hapa tunasubiri kuapishwa ili tuanze kazi kwa kuwatumia wananchi wetu waliotuchagua kwa kishindo, kuanzia Urais Dkt. John Magufuli, wabunge na sisi madiwani,” alisema Mkufya.

 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *