img

Joe Biden aja na sera mpya ya kigeni: Marekani imerudi

November 25, 2020

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema utawala wake utaimarisha jukumu la Marekani kama kiongozi wa dunia. Biden aliyesema hayo Jumanne wakati alipotangaza uteuzi wake wa kwanza wa baraza la mawaziri, akisisitiza kurejesha ushirikiano wa kimataifa. 

Biden amemteua Antony Blinken kuwa waziri wa mambo ya nje na John Kerry kama mjumbe wa mazingira. 

Biden anaamini kwamba Marekani itakuwa imara zaidi ikiwa itafanya kazi kwa karibu na washirika wake.

 Marekani imerejea na iko tayari kuongoza dunia, alisema Biden katika hafla hiyo. Mwelekeo mpya wa sera za kigeni wa Biden unaashiria tofauti na mwelekeo wa rais Donald Trump, wa Marekani kwanza, ambao ulimuweka kando na washirika wa jadi wa Marekani hasa Ulaya. 

Makamu wa rais mteule Kamala Harris ameongeza kuwa Marekani iko tayari katika mapambano ya tabia nchi.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *