img

India yapiga marufuku matumizi ya programu za simu za China

November 25, 2020

Programu 43 za simu zikiwemo 4 za kampuni kubwa za biashara ya mitandaoni za China pamoja na Alibaba Group zimepigwa marufuku nchini India kwa madai ya kuwa na athari kwa usalama wa taifa. 

Wizara ya Elektroniki na Mawasiliano imetoa maelezo na kubainisha sababu zilizopelekea marufuku hayo kwa kusema, “Programu hizi zimeonekana kuwa tishio kwa usalama wa taifa na kuvuruga taratibu za utendaji kazi wa umma.”

Serikali ya New Delhi pia iliwahi kupiga marufuku ya matumizi ya programu nyingi za simu mwezi wa Juni na Septemba kwa madai ya kuwa na athari ya usalama. 

Nyingi ya programu hizo zilizopigwa marufuku zinamilikiwa na China. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *