img

Breaking: Diego Maradona Afariki Dunia

November 25, 2020

MKONGWE wa Soka raia wa Argentina, Diego Maradona amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 60 kwa mshtuko wa moyo, leo Jumatano, Novemba 25, 2020, ikiwa ni wiki mbili tu baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya oparesheni ya ubongo.

 

Maradona atakumbukwa kwa umahili wake kwenye soka hasa alivyoisaidia timu yake ya Taifa ya Argentina kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1986. Amewahi kuchezea vilabu vikubwa duniani kama Boca Juniors, Napoli na Barcelona na kuwa tishio uwanjani huku akijikusanyia mamilioni ya mashabiki kila kona ya dunia.

 

Maradona atakumbukwa kwa bao lake la mkono liliopewa jina la ‘Hand of God’ katika mechi ya robo fainali kati ya Argentina na England lililoisaidia Argentina kuiondoa Uingereza kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka huo 1986, na kuibuka chuki kubwa dhidi yake na mwamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Tunisia.

 

Wiki mbili zilizopita Maradona alilazwa hospitali kwa tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo wake . Tatizo hilo madaktari walipambana nalo na kufanikiwa kuliondoa na kumruhusu arudi nyumbani.

 

Aliwahi kuwa ndani ya orodha ya wachezaji bora 100 wa FIFA wa muda wote lakini kipaji chake kilikuja kuharibiwa mwishoni baada ya kuwa mlevi wa pombe kupindukia.

The post Breaking: Diego Maradona Afariki Dunia appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *