img

Bieber Awakosoa Grammy Kuhusu Albamu Yake

November 25, 2020

Muimbaji wa muziki wa Pop na R&B kutokea nchini Canada Justin Bieber Mwaka huu Amepata nafasi ya kutajwa kuwania Tuzo za Grammy2021 katika Vipengele vinne ambavyo ni ‘Best Pop Vocal Album’, ‘Best Pop Solo Performance’, ‘Best Pop/Duo Group Performance’ na ‘Best Country Duo/Group Performance.’

 

Justine Bieber amewakosoa waandaaji wa tuzo hizo na Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bieber ameandika ujumbe akielezea kushangazwa na kitendo cha waandaaji wa hao kuiweka album yake ya ‘CHANGES‘ Kuwania Tuzo kwenye kipengele cha ‘Best pop vocal album’ wakati Albamu hiyo ni ya R&B.

 

Justin Bieber Amewataka Watu wasitafsiri vibaya alichokisema kwani hayo ni mawazo yake unaweza kukubaliana nayo au kuyakataa na Pia Amewashukuru watu wote Waliomuwezesha Kutajwa kuwania Tuzo katika Vipengele hivyo.

 The post Bieber Awakosoa Grammy Kuhusu Albamu Yake appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *