img

Zoezi la upigaji kura lakamilika na shughuli ya kuhesabu kura yaanza Burkina Faso

November 24, 2020

Shughuli ya kuhesabu kura imeanzishwa baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika hapo jana nchini Burkina Faso.

Uchaguzi huo wa urais na ubunge ulihusisha kati ya asilimia  38 na 40 ya washiriki waliosajiliwa, na matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa hapo kesho. 

Vituo 1,300 kati ya 21,000 vya upigaji kura havikufunguliwa kutokana na hofu ya usalama nchini humo , na watu 350,000 wakakosa kupiga kura. 

Takriban wananchi milioni 6.5 walijisajili kwenye uchaguzi huo uliohusisha wagombea 13 wa urais akiwemo Rais wa awamu ya mwisho Roch Marc Christian Kabore.

Wagombea 10,652 pia waliweza kushiriki kugombea nafasi za viti 127 vya ubunge. 

Kwa mara ya kwanza raia wanaoishi nje ya nchi wameweza kupiga kura kwenye uchaguzi. 

Jumla ya raia 23,108 wa Burkina Faso wanaoishi katika mataifa 22 walipata fursa ya kushiriki zoezi la upigaji kura kwenye vituo vilivyoundwa. 

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *