img

Yemen yakabiliwa na njaa kali

November 24, 2020

 Zaidi ya watoto milioni 12 wameripotiwa kuwa wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na njaa nchini Yemen.

Henrietta Fore, Rais wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti yake rasmi amesisitiza kuwa Yemen inakabiliwa na njaa mbaya zaidi.

Akibainisha kuwa “kengele za hatari zimekuwa zikilia kwa muda mrefu sana” kuhusu hali ya Yemen, Fore aliongeza kwa kusema,

“Zaidi ya watoto milioni 12 wanahitaji msaada wa kibinadamu.”

Akibainisha kuwa upungufu wa lishe umefikia kiwango cha juu katika maeneo mengine ya nchi, Fore, alionya,

“Zaidi ya watoto elfu 325 walio chini ya umri wa miaka 5 wanapigania maisha yao kutokana na utapiamlo.”

Fore amebaini kuwa zaidi ya watoto milioni tano nchini Yemen wako “katika hatari kubwa katika magonjwa ya kipindupindu na kuhara”.

Kiongozi huyo amekumbushia umaskini unaoendelea  nchini Yemen, pamoja na mizozo ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka mitano, vimepelekea watoto na familia zao kuwa katika ghasia na magonjwa.

Janga la Covid-19 limefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Akisisitiza kuwa UNICEF imekuwa ikifanya shughuli za misaada kwa Yemen kwa miaka, Fore amebaini kuwa shirika liliweza kukusanya dola milioni 237 tu kwa misaada ya kibinadamu mwaka huu, badala ya dola milioni 535 ambazo zinahitajika.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *