img

Tunakwenda bungeni kufanya kazi – Halima Mdee

November 24, 2020

Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Halima Mdee amewaahidi wanachama wa chama hicho kuwa wanakwenda bungeni kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge leo Jumanne Novemba 24, 2020 muda mfupi baada ya kula kiapo pamoja na wabunge wenzake 18, Halima ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) amesema, “nikushukuru kwa kiapo kufanyika na kukamilika, nikishukuru chama changu kupitia wao sisi tumepata nafasi hii ya kukiwakilisha chama chetu. Viti hivi sio hisani ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.”

 “Nikuhakikishie mheshimiwa spika tutafanya kazi kwa uaminifu kama kambi rasmi ya upinzani bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile tulivyokuwa tunavifanya. Kuna vijana wapya sisi kama dada zao tunakuhakikishia watafanya kazi bora. Niwahakikishie wana Chadema tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na uadilifu mkubwa sana.”

Amesema, “kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya nchi chama chetu kimekidhi kigezo vya kupata viti maalumu, viti hivi si hisani ila ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kimepata.”

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *