img

Trump Akubali Kukabidhi Madaraka kwa Biden

November 24, 2020

RAIS Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato rasmi wa kumkabidhi madaraka Rais Mteule Joe Biden kwa kuliambia shirika  linaloshughulikia mabadilishano hayo “lifanye kile kinachostahili kufanywa” hata wakati anaahidi kuendelea kupinga matokeo.

 

Ofisi ya utawala wa huduma za serikali imesema inamtambua  Biden kama “mshindi”. Hilo linawadia wakati  Biden ameidhinishwa rasmi kama mshindi wa jimbo la Michigan na kuwa pigo kubwa kwa Trump.

 

Timu ya  Biden imefurahishwa na kuanza kwa mchakato huo wakati Rais Mteule anajiandaa kwa sherehe za kuapishwa Januari 20.

The post Trump Akubali Kukabidhi Madaraka kwa Biden appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *