img

Tanzania yateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

November 24, 2020

 Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, kwa mwaka 2020/2021, Uteuzi huu ulipendekezwa na Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuteuliwa kwa kauli moja na wajumbe wote wa kamati hiyo.

Tarehe 23 Novemba 2020, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Prof. Kennedy Gastorn, ameongoza kikao cha kwanza cha kamati hii kwa mwaka huu, hii ni mara ya kwanza Tanzania kushika nafasi ya kuongoza kamati hii nyeti ya Umoja wa Mataifa.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *