img

RC Kunenge Awapongeza Wauguzi Dar

November 24, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewapongeza Wauguzi wa Mkoa huo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya Katika kuokoa maisha ya wananchi jambo lililosaidia kupunguza vifo.

 

RC Kunenge amesema hayo leo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Mkoa wa Dar es salaam ambapo amewahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa uwezo wao wote na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega.

Aidha, RC Kunenge amesema Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuboresha huduma za Afya kupitia Ujenzi wa hospital, zahanati, vituo vya Afya na kununua Vifaa tiba ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.

 

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema anafurahi kuona hata zile kelele za wananchi kuhusu lugha chafu zimepungua na badala yake saivi Wauguzi wamekuwa na lugha za upendo kwa wagonjwa jambo linalotia faraja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dr. Rashid Mfaume amewaalika wananchi kujitokeza kwenye Viwanja vya Karimjee kujionea kazi zinazofanywa na Wauguzi wa Mkoa huo.

 

Aidha, Dkt. Mfaume amewaahidi wananchi kutegemea mabadiliko makubwa Katika sekta ya Afya kwakuwa Serikali ya Mkoa imejidhatiti vizuri kutoa huduma Bora na zenye tija.

 The post RC Kunenge Awapongeza Wauguzi Dar appeared first on Global Publishers.

,

Article Categories:
Uncategorized

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *